28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tambwe: Maximo, Coutinho hawanitishi

Amis Tambwe
Mshambuliaji wa Simba SC, Amis Tambwe

NA SAADA AKIDA, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Amis Tambwe, ameanza rasmi mazoezi na timu hiyo jana na kusema ujio wa kocha wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo na mshambuliaji, Andrey Coutinho, haumshtui na wasubiri watakapokutana katika msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tambwe amejiunga na kikosi cha timu hiyo akitokea mapumzikoni na kuanza mazoezi ya gym na wenzake kujiandaa na ligi hiyo, itakayoanza Septemba 20 mwaka huu.

Akizungumza jana, Tambwe alisema hajawahi kumuona Maximo akifundisha wala Coutinho akicheza, kwani hatishwi na kuhakikisha mpira utaonekana uwanjani.

Alisema anachokiangalia zaidi ni kuhakikisha anafanya kazi iliyomleta Simba, kwa kutohofia wapinzani wao wamesajili wachezaji kutoka nchi gani.

“Si kila anayetoka Brazil anaweza kila kitu katika soka, kikubwa upande wetu tutahakikisha tunajipanga kufanya vyema katika maandalizi ya kuleta raha siku tutakayokutana nao,” alisema Tambwe.

Alisema Yanga kuajiri makocha na kiungo kutoka Brazil, haimaanishi wanaweza kufanya vizuri msimu ujao wa ligi, kwani hata Brazil iliondolewa katika nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia.

“Wanasimba wasihofie ujio wa Maximo na Coutinho, kwani si kila anayetoka Brazil ndio anaweza kucheza soka safi, kikubwa ni maandalizi maana hata Brazil iliondolewa katika nusu fainali kwa mabao 7-1,” alisema Tambwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles