29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Maximo ampa Coutinho majukumu Yanga

Coutinho wa yanga
Coutinho wa yanga

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

KOCHA wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo, ameanza kumuandaa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Andrey Coutinho, kuwa mpiga kona za upande wa kushoto wa timu hiyo.

Coutinho ambaye awali alikiri kutumia zaidi mguu wa kushoto kuliko wa kulia, alianza kupewa majukumu hayo jana katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Loyola jijini Dar es Salaam na kutimiza vema majukumu yake hayo.

Katika mazoezi hayo yaliyoanza kwa Maximo kuwapa mazoezi ya kupigiana pasi wachezaji wawili wawili, kwa ajili ya kuwajengea stamina na kuwagawa katika timu mbili huku akiwataka wacheze kwa haraka.

Timu moja ilidakiwa na kipa, Juma Kaseja na nyingine ikiwa na kipa Ally Mustapha ‘Bathez,’ ambapo timu ya Kaseja iliyokuwa ikiongozwa na wachezaji Nizar Khalfan, Jerryson Tegete, Andrey Coutinho, Abdul Juma ilitundikwa mabao 2-0 na timu aliyokuwa akiidakia Barthez iliyokuwa na wachezaji wa timu B wakiwa na Juma Javu, Omega Seme na wengineo.

Katika mazoezi hayo, Coutinho alionyesha kuendelea kutekeleza jukumu lake alilopewa na kocha huyo, kwa kuwa ndio mchezaji tegemezi kwenye timu yake kupiga kona kali ambayo kama inapata wamaliziaji wazuri, lazima wafunge bao.

Yanga sambamba na kufanya mazoezi ya uwanjani asubuhi, lakini jioni hufanya pia mzoezi ya viungo ili kujiweka fiti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles