27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tamasha la Lakwetu Concert Family kutoa tuzo

kwetu family Ester (1)NA GEORGE KAYALA

WARATIBU wa tamasha la Lakwetu Concert Family 2016, wanatarajia kutoa tuzo kwa watu waliochangia kwa kiasi kikubwa kuibua na kukuza waimbaji wengi wa nyimbo za injili nchini wakiwemo wachungaji na maaskofu wa makanisa mbalimbali.

Msemaji wa tamasha hilo, Ester Marthias, alisema lengo ni kuwatia moyo na kuthamini mchango wao wa kuibua waimbaji chipukizi wa muziki huo.

“Dhumuni la tamasha hili ni kuwainua waimbaji wasiojulikana na kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘albino’, pia kutoa tuzo kwa waliofanikisha kukuza sekta hii ya muziki wa injili ili kuwatia moyo na kutambua thamani yao,” alisema Ester.

Tamasha la kwanza litafanyika Julai 3, mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na litafuatiwa na kufuatiwa na mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles