24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

John Legend, Chrissy wapata mtoto wa kike

John Legend na Chrissy TeigenNEW YORK, MEREKANI

MSANII wa muziki wa RnB, John Legend na mke wake, Chrissy Teigen, wamekuwa na wiki ya furaha kwao baada ya kufanikiwa kupata mtoto wa kike mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kupitia akaunti ya Instagram ya Legend, aliweka wazi jina la mtoto huyo na kumpongeza mke wake kwa kupata mtoto salama.

“Tunamshukuru Mungu, tumefanikiwa kupata mtoto wa kike anayeitwa, Luna Simone Stephens, tumekuwa na wiki ya furaha kutokana na ugeni huo, nampongeza mke wangu kwa uvumilivu katika kipindi chote,” aliandika Legend.

Huyu ni mtoto wao wa kwanza katika familia, hivyo msanii huyo amedai kwamba anatarajia kujifunza maisha ya kuilea familia yake.

“Sasa tumekuwa na mgeni katika familia, natarajia kuonekana baba bora kwa kuonyesha malezi mazuri kwa mtoto na mama yake,” aliongeza Legend.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles