28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Diamond kuiwakilisha Afrika Mashariki tuzo mpya

Diamond PlatnumNA HERIETH FAUSTINE

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassibu Abdul ‘Diamond Platnum’, amechaguliwa kuwania tuzo iitwayo African Culture Image 2016 (ACI) ambazo ni kwa ajili ya wasanii wa Afrika.

Diamond amekuwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki kutajwa kuwania tuzo hizo zinazotolewa na Wanaigeria na katika tuzo hizo ametajwa katika kipengele cha msanii bora wa kiume wa mwaka.

Wasanii wengine waliotajwa kuwania kipengele hicho ni pamoja na wasanii kutoka Nigeria; Wizkid, Davido, Kcee, Patoraking na Olamide.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa mwaka huu nchini Marekani katika jimbo la Antalnta Georgia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles