27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Ney wa Mitego kutoka kivingine Juni

NayWaMitegoNA MARTIN MAZUGWA

BAADA ya wimbo wake wa ‘Shika Adabu Yako’ kukumbwa na changamoto mbalimbali mwana hip hop, Emanuel Elibariki (Ney wa Mitego), yupo mbioni kuachia wimbo mpya ili kuwaweka sawa mashabiki wake wanaomfikiria tofauti.

Wimbo huo utatoka kati ya Juni 6 na 9 na lengo ni kuwarudisha mashabiki wake walioanza kumchukulia tofauti baada ya kutoa wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ulioelezwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwamba umekiuka maadili.

“Baada ya Basata kufungia wimbo wangu sitaki kuwasononesha mashabiki wangu, ndio maana nimeamua kuwaletea kitu kipya naamini watakipenda.

“Kazi yangu ni muziki hivyo mashabiki wangu na wapenzi wa muziki wa hip hop wakae mkao wa kula kama wanavyonijua huwa sikosei katika kazi zangu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles