25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Tamasha fahari ya Mwafrika kufanyika Oktoba 3

FahariTUNU NASSOR NA LUGOLA CHITAGE (TUDARCO)
TAMASHA la Fahari ya Mwafrika litakaloshirikisha wadau wa sanaa ya mitindo, vichekesho na wapishi wa vyakula vya asili linatarajiwa kufanyika Oktoba 3 mwaka huu.

Mkurugenzi wa kampuni ya Black Sensation ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, Lilian Masuka, alisema tamasha hilo litakalofanyika Escape One linalenga kukuza mila na tamaduni za Kiafrika zinazoelekea kupotea nchini.

“Washindi wa shindano hili hawatachaguliwa kwa kupigiwa kura bali tafiti zitakazofanywa kwa washiriki ndizo zitaonyesha nani anastahili tuzo kutokana na kazi atakayoifanya,’’ alisema Lilian.

Katika tamasha hilo pia taasisi mbalimbali ikiwemo Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Tasuba), Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), wanamitindo na wasanii mbalimbali akiwemo Barnaba na bendi ya Skylight wakishirikishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles