25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Christian Bella awa kiburudisho sherehe ya Tiffah

IMG-20150921-WA0004NA CHRISTOPHER MSEKENA

MASTAA wengi wamejitokeza kuiona sura ya mtoto wa msanii, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, anayeitwa Lattifah ‘Tiffah’ baada ya kutimiza siku 40 tangu alipozaliwa.

Baadhi ya mastaa waliohudhuria katika sherehe ya kutolewa mtoto huyo ni Aunt Ezekiel, Mrisho Mpoto, Queen Dareen, Shetta, Christian Bella, Dj Ommy na wengine wengi.

Msanii Christian Bella ndiye alikuwa mtumbuizaji mkuu katika sherehe hiyo na kukonga nyoyo zao hasa alipoimba wimbo wa ‘Ukimuona’, ambao ni remix ya wimbo ulioimbwa na baba wa mtoto huyo.

Mtumbuizaji mwingine alikuwa baba wa mtoto huyo, Diamond.

Hata hivyo, mtoto huyo ameonekana kupata umaarufu kwa kasi kutokana na matukio mbalimbali ya wazazi wake na tuhuma mbalimbali zilizowakumba wazazi hao katika uhusiano wao wa kimapenzi waliopitia kabla ya kukutana kwao na hadi walipopata mtoto huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles