26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

TAKUKURU yafuta madeni ‘feki’ ya Sh milioni 294

Na Nyemo Malecela, Bukoba

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Kagera imefanikiwa kurejesha zaidi ya Sh milioni 10.3 katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na kuwezesha kufuta madai batili yenye thamani ya Sh milioni 294.23 yaliyokuwa yameandaliwa na maduka ya dawa ya MK Pharmacy na EJU Enterprises ili kufanya ubadhilifu wa fedha katika mfuko huo.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera, John Joseph amesema jana kuwa madai hayo ya uongo yalikuwa ya Mei hadi Novemba 2016 yaliyotoa dawa kwa wagonjwa, ambayo yaliandikwa na mtu anayefahamika kama, Frida Samwel ambaye si daktari.

Hata hivyo Frida pamoja na kuwa Daktari hakuwahi kuajiriwa katika taaluma hiyo katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera na hatambuliki.

“Kwa maana hiyo nyaraka hizo zilikuwa zimegushiwa na duka la madawa la MK Pharmacy linalomilikiwa na Murtaza Pathan na EJU Enterprises linalomilikiwa na Erick Kiiza zilikuwa zimegushiwa na ziliandaliwa kwa nia ovu ya kutaka kufanya udanganyifu.

“Duka la MK Pharmacy liliwasilisha madai hewa katika mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya yenye thamani ya Sh milioni 231.99 na kulipwa Sh milioni 10.19 wakati EJU Enterprises liliwasilisha hati ya madai yenye thamani ya Sh milioni 72.60 na kulipwa kiasi cha Sh 169,800,” amesema Joseph.

Pamoja na fedha hizo kurejeshwa pia Takukuru imefanikiwa kurejesha kiasi cha Sh 9,964,494.62 kutoka kwa wadaiwa sugu na kuingizwa katika akaunti maalum ya ukusanyaji wa madeni ya Benki ya wakulima (Kagera Farmers Cooperatve Bank).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles