26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

DAWASA yatakiwa kufikisha maji kwa wananchi wa pembezoni

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mbunge wa Kibamba (CCM), Issa Mtemvu ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kukamilisha kazi ya kufikisha maji kwa wananchi hususan waliopo pembezoni kwa kuwaunganisha kwenye mtandao wa maji ili kuharakisha upatikanaji wa huduma maji na kupunguza malalamiko.

Mtemvu ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA kwa lengo la kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi ipasavyo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika kwenye kata za Kawe, Ubungo na Kibamba, Mtemvu amesema utekelezaji wa miradi ya maji kwa maeneo yote unaendelea vizuri.

“Hatahivyo, tumebaini uwepo wa changamoto mbalimbali zinazochelewesha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi,”

Amebainisha kuwa ziara hiyo imetokana na majadiliano yaliyotokana na kikao kazi cha, Waziri wa Maji na wabunge wa Dar es Salaam na Pwani kilichofanyika hivi karibuni chini ya Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Mtemvu amesema bado kuna changamoto ya upatikanaji wa maji kwenye maeneo aliyotembelea, hususani kata ya Kibamba ambayo ipo pembezoni.

“Tumebaini kuna kazi ndogo iliyobaki ya kukamilisha maunganisho ya maji toka kwenye mtandao mkuu wa maji kwenda kwa wananchi na hivyo kuchelewesha upatikanaji wa maji kwa wananchi.

“Tunatambua kuwa ipo nia njema kwa DAWASA kuanzia kwa Mtendaji Mkuu na Mameneja wote ya kutatua changamoto za maji, tunaamini kazi iliyobaki ya kukamilisha maunganisho ya mabomba toka kwenye mtandao mkuu kwenda kwenye nyumba za wananchi itakamilika na wananchi watapata maji kikamilifu,” amesema Mtemvu.

Ameongeza kuwa ipo kazi kubwa inayofanyika ya utekelezaji wa miradi mikubwa inayoenda kumaliza changamoto ya maji kwa kata ya Kibamba, Ubungo na Kawe.

“Tunaimani kubwa na watendaji wa Mamlaka kwamba wataenda kufanya kazi ya kutatua changamoto zilizoonekana kwenye maeneo yaliyopitiwa,” amesema.

Mtemvu ameongeza kuwa ziara imempa kujifunza namna DAWASA inavyojitahidi kushughulikia tatizo la upatikanaji wa maji kwenye sehemu korofi kwa kutumia njia ya mbadala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles