22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Watatu wapoteza maisha kwa kukanyangwa na tembo Karagwe

Na Nyemo Malecela, Bukoba

Watu watatu wa familia moja wilayani Karagwe wamepoteza maisha na mmoja kujeruhiwa na tembo wanaodaiwa kuvamia makazi ya wananchi katika kijiji cha Nshabaiguru kata ya Kihanga wilayani humo.

Watu waliopoteza maisha katika tukio hilo ni Fredy Muhile (40) kibarua wa kuchunga ng’ombe na baba wa familia, Aneth Fredy (33) mama wa familia na mtoto wao Angel Fredy (1.5) na majeruhi ni Juma Rashid (18) kibarua wa kuchunga ng’ombe.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocutus Malimi amesema tukio hilo lilitokea Januari 3, mwaka huu saa 11.45 katika kitalu namba tano cha pori la malisho linalomilikiwa na Salvatory Wamara ambalo linapatikana katika hifadhi ya Taifa ya Rumanyika.

 “Marehemu Aneth alikuwa anaelekea kisimani kuchota maji akiwa amebeba mtoto mgongoni ndipo gafla alikutana na kijana wa kijijini hapo aliyekuwa anafukuzwa na tembo mmoja kati ya kundi la tembo lililovamia kijijini hapo, tembo huyo alimvamia mama huyo na mwanae na kumjeruhi.

“Mama na mtoto walikimbizwa katika hospitali ya Nyakahanga na kulazwa lakini Januari 3, mwaka huu wote wawili walifariki wakati wakipatiwa matibabu.

“Aidha Fredy ambaye ni mume wa Aneth alipopata taarifa ya famliia yake kushambuliwa na tembo aliondoka na kwenda porini kwa ajili ya kutoa msaada kwa familia yake lakini alikutana na tembo huyo akamshambulia na kusababisha kifo chake hapohapo na mwili wake uligundulika kesho yake,” amesema RPC Malimi.

Malimi amesema majeruhi bado yuko Hospitali anaendelea na matibabu na kuwataka wananchi wanaoishi vijiji vya kando ya hifadhi kuchukua tahadhari au kahama kuwa mbali na maeneo yanayoweza kufikwa na wanyama hao wanaofuata mazao yanayolimwa kama vile maembe na mahindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles