24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TAKUKURU waokoa kiwanja cha CCM Kiteto

Na Mohamed Hamad, Kiteto

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) wilayani Kiteto mkoani Manyara, imerejesha kiwanja cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Bwagamoyo kilichokuwa kimeporwa na Mwenyekiti wa kata hiyo, Charles Mbaluk.

Akizungumza leo Jumatatu Desemba 14, Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Kiteto, Venance Sangau amemweleza Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Kanali Patrick Songea katika makabidhiano hayo kuwa walipata malalamiko toka kwa wanachama wa CCM kata ya Bwagamoyo kuporwa Kiwanja hicho.

Amesema baada ya uchunguzi walibaini kuwa mwenyekiti huyo alijimilikisha sehemu ya kiwanja hicho chenye ukibwa wa mita 930.776 toka mwaka 2015 kilichoko mtaa wa msente na kujenga nyumba yake na kuuza sehemu kwa Sh 700,000.

Amesema kiwanja hicho kilitolewa na serikali ya Kijiji cha Bwagamoyo baada ya kuombwa na Chama hicho ili wajenge ofisi ya chama toka mwaka 2013 lakini kiongozi huyo alihodhi na kukitumia kwa maslahi yake binafsi.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Manyara, Holle Makungu aliyeshughudia makabidhiano hayo ametoa rai kwa CCM Wilaya kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa kiongozi huyo, Charles Mbaluka ambaye pamoja na kitendo cha kukihujumu chama bado yeye ni kiongozi.

Ameshauri baraza la wadhamini la CCM kuendelea kuzitambua mali za chama hicho vikiwamo viwanja na kuhakikisha vinakuwa na hati miliki ili kuepuka kuporwa na watu wasio waadilifu

Akikabidhi kiwanja hicho Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Kanali Songea ameonya tabia hizo na kutaka wananchi kuendelea kutoa ushirikiani kwa Taasisi ya Takukuru pamoja na Serikali

Amesema Takukuru wamefanya kazi kubwa Kiteto na ya kihistori kwani mbali na mali za chama na serikali hata watu binafsi wamekuwa wakirejeshewa haki zao zilizokuwa zimepotezwa.

upande wake, Mwenyekiti wa CCM Kiteto, Mohamed Kiyondo akikabidhiwa kiwanja hicho amesema atamwagiza Katibubwa CCM wilaya kumwandikia barua mwenyekiti huyo wakati taratibu zingine za kinidhamu zikiendelea kufuatwa.

Nao baadhi ya wanachama wa CCM kata ya Bwagamoyo wameshukuru Taasisi hiyo wakusema wasingepata haki yao hiyo kwani ilikuwa vigumu kukipata baada ya kushindikana kufuatiliwa wilaya na mkoani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles