27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

TAKUKURU KUWASHUGHULIKIA WATAKAOINGIA TFF KWA RUSHWA

Na ASHA MUHAJI – DODOMA

TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa  (Takukuru), imeahidi kuwashughulikia wagombea watakaobainika wametumia rushwa kuingia madarakani.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Mussa Chaulo, alitoa kauli hiyo jana kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), katika Ukumbi wa Hoteli ya St Gasper, mjini Dodoma, ulipofanyika uchaguzi huo.

Chaula alisema tayari wanazo taarifa za baadhi ya wagombea walioshiriki kinyang’anyiro hicho kujihusisha na vitendo hivyo vya rushwa na kwamba kwa sasa bado wanazifanyia kazi taarifa hizo.

Mkuu huyo wa Takukuru amewatoa hofu wajumbe hao kuwa kukamilika kwa uchaguzi si sababu ya kufungwa kwa zoezi hilo.

“Wote waliolalamikiwa kujihusisha na rushwa bado wanafuatiliwa hadi sasa, hivyo mtasikia tu,” alisema.

Takukuru imeahidi kuendelea kufuatilia vitendo vya rushwa pia katika masuala mengine yanayohusiana na michezo, ukiwamo huu wa soka.

Chaulo alitaja baadhi ya sehemu iliposhamiri, ukiacha katika chaguzi ni  mikataba, upangaji wa ratiba za mashindano, manunuzi ya vifaa pamoja na kwenye matumizi mabaya ya fedha yatokanayo na mapato na matumizi ya taasisi husika.

Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, aliwataka wajumbe wachague viongozi watakaokuwa na maono na malengo kuinua soka la vijana.

Dk. Mwakyembe alisema jukumu la kwanza la TFF ni kuhakikisha wanaitunza vema timu ya vijana iliyofuzu kucheza fainali za vijana za Afcon mwaka huu ‘Serengeti Boys’, ambayo sasa imebadilishwa na kuwa Ngorongoro Boys.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles