29.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 30, 2024

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Takukuru Dodoma yabaini uchepuzi wa vifaa vya ujenzi wa miradi

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imesema miradi 19 imebainika kutekelezwa kwa kiwango stahiki lakini wamebaini uchepuzi wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 40 kwenye mradi mmoja.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa Julai 2, 2021 Kamanda wa Takukuru mkoa wa Dodoma, Sostenes Kibwengo amesema katika uchunguzi wao wamebaini miradi 19 kutekelezwa kwa kiwango stahiki na uchepuzi wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 40 kwenye mradi mmoja.

“Ufuatiliaji wetu umewezesha kuokoa na kudhibiti jumla ya Sh milioni 215.66 ambazo zingepotea kwa kuchepushwa, kufujwa au kulipwa kwa watu wasio stahili kinyume nataratibu,”amesema.

Amesema kuwa sekta nyingine ni za  binafsi asilimia 7, Elimu, Afya na Polisi asilimia 6 kila moja.

Hata hivyo amewataka  watumishi waliopo katika sekta zinazolalamikiwa zaidi kwa rushwa katika mkoa wa Dodoma kujitafakari kwani siku za mwizi ni arobaini.

Katika hatua nyingine Takukuru mkoani humo imefanikiwa kuokoa na kudhibiti zaidi ya Sh milioni 200 ambazo zingepotea kwa kuchepushwa kufujwa ama kulipwa kwa watu wasiostahili kinyume na utaratibu.

Amesema ufuatiliaji wa Takukuru umewezesha kudhibiti fedha hizo ambazo zilitakiwa kulipwa kinyume cha  utaratibu.

Kamanda Kibengo ametolea mfano wa uchepushaji wa gari la Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma ambalo lilipata ajali na kupelekwa gereji moja jijini Dodoma ambapo ilibaini vifaa 101 vyenye thamani ya Sh milioni 87,785,000 vilichepushwa kutoka kwenye gari hilo.

“Kwa kushirkiana na Temesa ikabainika kwamba vifaa 101 vyenye thamani ya Sh 87,785,000 vilichepushwa kutoka kwenye gari hilo hadi tulipoingilia  na kuwezesha vifaa hivyo kurejeshwa,”amesema.

Mkuu huyo wa Takukuru mkoa amewataka wamiliki wa gereji binafsi mkoani dodoma wenye tabia ya kuchepusha na kubadilu vipuli vya magari ya umma wanayoletewa kwaajili ya matengenezo waache tabia hiyo kwani wanafatilia na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakao bainika.

Aidha, Kamanda Kibwengo amesema kuwa miradi 20 ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 1.775 katika sekta ya elimu, afya na ujenzi ilikaguliwa kwa lengo ka kujiridhisha iwapo thamani halisi ya fedha imepatikana kwa kuangalia iwapo kuna ufujaji.

Pia, amesema kuwa wamefanya chambuzi 6 za mifumo ya utendaji na utoaji huduma katika sekta za ardhi, elimu, mapato na ujenzi ambapo mianya ya rushwa ilibainishwa.

“Baadhi ya chambuzi zilizofanyika  ni rushwa na udanganyifu katika mitihani katika baadhi ya vyuo ambapo imebainika kuna baadhi ya wahadhiri na watumishi wengine wa vyuo wanashirikiana na wanafunzi kufanya udanganyifu katika mitihani,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles