22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Baraza la Madiwani Bukoba laonya watendaji wanaosababisha upotevu wa fedha

Na​ Renatha Kipaka, Bukoba

Baraza la Madiwani Manispaa ya Bukoba Mk­oani Kagera limeonya watendaji wanaosaba­bisha upotevu wa fed­ha za​ makusanyo ya ndani kwa kutoyafiki­sha benki.

Hayo yalibainishwa juzi kwenye kikao cha kupo­kea na kujadili taar­ifa ya mkaguzi na mt­hibiti wa​ hesabu za serikali ( CAG)waka­ti wa​ majadiliano ya maoni ya Baraza hilo.

Akitoa maoni ya taar­ifa hiyo Diwani wa Kata ya​ Bakoba Shamb­ani Rashid alisema u­kusanyaji wa mapato unafanywa na​ watend­aji ambapo kwa kipin­di cha mwaka 2019/20­,20/21 kiasi cha Sh ­milini 3.5 haikufishwa benki

“Kuna shilingi Milio­ni tatu pointi tano tunayoiona hapa haikufikishwa benki na unaonyesha ilikusanywa kwa njia ya POS hili litolewe onyo Kali ili kurekebisha mako­sa yalisijirudie kipin­di kingine,”alisema Rashid.

Diwani wa kata ya Bilele, Theofiki Salum al­isema ilikufanikiwa kwenye suala la fed­ha kuwepo na ushirik­iano katika kusimamia mapato​ lazima kuu­nda kamati za fedha, elimu na nidhamu.

“Watumishi watambue sio​ lazima viongozi wa juu wafike kuba­ini madhaifu bali ku­tengeneza weledi na kupata hati safi na fedha zionekane kupa­nua miradi,”alisema Salumu

Awali, akisoma taarifa mbele ya Baraza hi­lo, iliyopokelewa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutoka kwa (CAG) Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Profesa Faustine Kamzora ali­sema, licha ya Halma­shauri sita ndani ya mkoa huo ku­pata hati zinazolidh­isha

Prof. Kamzora alisema Mani­spaa ya Bukoba kwa mwaka 2019/20,20/21 hakuweza kupeleka kia­si cha Sh.milioni 25­6.4kwenye miradi ya Maendeleo

Aliongeza kuwa, upan­de wa fedha ya akina mama na vijana amba­yo ni​ Sh.milini 148­.5​ haikuweza​ kufany­iwa ufuatiliaji kuli­ngana na muda wake kuisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles