24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

TAFITI ZINAHITAJIKA KUJUA KIWANGO CHA ATHARI ZA TUMBAKU

NA VERONICA ROMWALD-ALIYEKUWA KENYA

TAFITI za kina kubainisha kiwango cha athari za kiafya kwa bidhaa zitokanazo na tumbaku bado zinahitajika kufanyika Barani Afrika ili kuielimisha jamii na kuzihamasisha serikali kuanza kuchukua hatua, imeelezwa.

Hayo yalielezwa hivi karibuni nchini Kenya na Mwanzilishi na Rais wa Shirika lisilo la Kiserikali la Leadership Impact Dynamics, Ade Adeyami alipowasilisha mada kwenye warsha maalum kwa waandishi wa habari hasa wajibu wao katika kuwezesha nchi kufikia lengo namba tatu la Malengo Endelevu ya Dunia (SDGs).

“Matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kati ya mwaka 2010 na 2011 vijana wa umri wa kati ya miaka 13 hadi 15 Barani Afrika walionekana kuwa wameanza kutumia bidhaa hizo,” alisema.

Alisema pamoja na utafiti huo bado kuna haja ya kufanya nyingine nyingi zitakazosaidia kwa namna moja au nyingine kuokoa kizazi cha Afrika.

“Kama hali ilikuwa hivyo unaweza kutafakari tupo wapi sasa na tunaelekea wapi, jamii inahitaji kupatiwa elimu ya kutosha kuhusu athari zitokanazo na matumizi ya bidhaa hizo, kwa hali ilivyo sasa.

“Ikiwa juhudi hazitachukuliwa basi itakuwa vigumu kufikia lengo namba tatu la Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani (SDGs) ambalo linahimiza afya bora kwa wote,” alisema.

Alisema takwimu zinaonesha kiwango cha matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku duniani ni kikubwa kulinganisha na mabara mengine.

“Inakadiriwa kufikia mwaka 2025 kutakuwa na watumiaji wa bidhaa zitokanazo na tumbaku kufikia bilioni moja,” alibainisha Adeyemi.

Akizungumza, Magesha Ngwiri alisema takwimu zinaonesha bara hilo kiwango cha matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku kwa sasa kipo kwa asilimia 80.

“Takwimu za WHO zinaonesha kila mwaka watu milioni saba hufariki dunia kutokana na matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku na idadi hiyo inakadiriwa kuwa itaongezeka mara dufu,” alisema.

Naye Mhadhili na Mwanachama wa Kudumu wa Taasisi ya Biashara ya Gordon, Chuo Kikuu cha Pretoria, Dk. Tendai Kadenhe Mhizha, alisema kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa (UN) zilizotolewa mwaka 2012 zinaonesha vilitokea takriban vifo milioni 38 duniani.

“Asilimia 68 ya vifo hivyo vilitokana na magonjwa yasiyo kuwa ya kuambukiza, unaweza kwa mantiki hiyo ni muhimu wanahabari kujikita zaidi kuelimisha jamii juu ya athari ili kushawishi serikali pia kuweza kuchukua hatua kukabiliana na jambo hili,” alisisitiza.

Warsha hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Oxegene imefanyika Novemba 22, mwaka huu nchini humo ambapo waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali wameshiriki na kujadiliana.

Nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Kenya, Malawi, Zimbambwe, Uganda, Rwanda, Zambia, Botswana, Swaziland, Lesotho, Ethiopia, Mozambique na Afrika Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles