24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

LUKUVI AMPA AGIZO MKURUGENZI WA TEHAMA

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Na JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAM

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Tehama wa wizara hiyo, Shabani Pazi, kuhakikisha hadi kufikia Juni mosi 2018 mfumo wa unganishi wa taarifa za ardhi uwe umekamilika na kuanza kufanya kazi.

Lukuvi alitoa agizo hilo Dar es Salaam jana alipotembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha kutunza kumbukumbu kwa njia ya kielekroniki ambacho kinafadhiliwa na Benki ya Dunia wenye lengo la kuimarisha usalama katika umiliki wa ardhi.

Alisema huo unatarajia kuanzia katika Manispaa za Wilaya ya Ubungo na Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo baadaye katika awamu ya pili itaunganishwa mikoa mingine ili kuondoa migogoro ikiwa ni pamoja na changamoto ya umilikishaji wa ardhi kwa mtu zaidi ya mmoja (double standard).

“Nimemwagiza kuanzia Juni mosi mwakani hati mpya kwa njia ya kijigitali zianze kutolewa hususani katika wilaya ambazo mradi unaanzia, kwa watu wenye hata za zamani wataweza kuzibadilisha bure. Pia tunatarajia kupitia mradi huu mchakato wa  utolewaji wa hati utakuwa wa haraka zaidi kwani hata kwa siku moja hadi saba mtu anaweza kuipata.

“Hizi zote ni juhudi za Serikali katika kuboresha mfumo wa uhifadhi wa taarifa za ardhi kutoka mfumo wa kutumia mafaili hivyo kituo hiki kitaunganisha taarifa zote za ardhi kutoka Idara ya Mipango miji, upimaji, usajili, ardhi, uthamini na kuziingiza mtandaoni,” alisema Lukuvi.

Alisema kupitia mumo huo vitendo vya udhalilishaji, wizi na udhalimu vitakomeshwa kwani hakuna Afisa ardhi ambaye ataweza kuingia kwenye mfumo kuangalia taarifa sipokuwa mkurugenzi pekee.

Alisema hatua hiyo itasaidia serikali kupata kodi halali kutoka kwa wamiliki wa ardhi kwani kutokana na mfumo uliopo inashindwa kufanya hivyo kwani wapo watu waliopata hati kabla ya uhuru jambo linalopelekea taarifa zao kushindwa kuonekana hivyo kukosa namna ya kuwatambua na kuwatoza kodi.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Tehama, Shaban Pazi, alisema hadi wakati huu ramani za mipango miji takribani 2800 zimeshabadilishwa kutoka kwenye mafaili hadi katika mfumo wa kidijitali huku ramani 13,575 zikiwa tayari zimeskaniwa ili kuwekwa kwenye mfumo huo.

“Kukamilika kwa mfumo huu utasaidia kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu za ardhi, kupunguza muda wa kusajili hati miliki, kupunguza siku za kusajili miamala (mortgages),” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles