Mwandishi Wetu, Arusha
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), imewataka wadau wake wote wanaomiliki na kutumia vyanzo vya mionzi hapa nchini kuhakikisha wanalipia leseni zao za mwaka 2019/20.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha TAEC, Peter Ngamilo jijini Arusha jana Mei 28, ambapo amesema leseni za wadau hao zinaishia Juni 30, mwaka huu.
“Wadau wote wa TAEC wanatakiwa kuhakikisha wanapata leseni mpya na ambao hawatakata leseni watakuwa wanafanya biashara kinyume na sheria ya Nguvu za Atomiki Tanzania namba 7, ya mwaka 2003,” amesema Ngamilo.
Aidha, Ngamilo pia amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaoshindwa kutii agizo hilo.