TAEC yawakumbusha wadau wa mionzi kukata leseni mpya

0
1321

Mwandishi Wetu, Arusha

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), imewataka wadau wake wote wanaomiliki na kutumia vyanzo vya mionzi hapa nchini  kuhakikisha  wanalipia leseni zao za mwaka 2019/20.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha TAEC, Peter Ngamilo jijini Arusha jana Mei 28, ambapo amesema leseni za wadau hao zinaishia Juni 30, mwaka huu.

“Wadau wote wa TAEC wanatakiwa kuhakikisha wanapata leseni mpya na ambao hawatakata leseni watakuwa wanafanya biashara  kinyume na  sheria ya Nguvu za Atomiki Tanzania namba 7,  ya mwaka 2003,” amesema Ngamilo.

Aidha, Ngamilo pia amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaoshindwa kutii agizo hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here