31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Alphonce Simbu achemka nchini Marekani

MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

Mwanariadha nyota wa Tanzania, Alphonce Simbu na wenzake kutoka hapa wamefanya vibaya katika mashindano ya mbio za Bolder Boulder, yaliyofanyika juzi nchini Marekani.

Katika mashindano hayo Simbu ameshika nafasi ya 14 akimaliza kwa dakika 30:16 huku watanzania wengine, Andrew Panga akimaliza nafasi ya tatu akitumia dakika 29:09 na Gabriel Geay akimaliza wa tano akitumia dakika 29:13.

Kwa upande wa wanawake, Magdalena Shauri alimaliza katika nafasi ya nane akitumia dakika 34:05 huku Natalie Elisante akitumia dakika 35:13 akimaliza katika nafasi ya 14.

Simbu amesema anamshukuru Mungu kwa kushika nafasi hiyo kwani mbio hizo zilikuwa na ushindani mkubwa tofauti na alivyofikiria.

“Wenzetu walikuwa wamejipanga vyakutosha tofauti nasisi maandalizi yetu hayakuridhisha, tutajipanga tena kwa ajili ya mbio nyingine,” amesem Simbu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles