28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

TAEC yaonya matumizi simu iliyokwisha chaji

Asha Bani, Dar es Salaam

Watanzania wametakiwa kutotumia simu ikiwa imeisha chaji au ikiwa inachajiwa, kwani husababisha madhara ikiwamo kusababisha kichwa kuuma.

Aidha, wazazi wameshauriwa kutowapa watoto wadogo simu janja (smart phone) kutumia muda mrefu kwani inaweza kuwaathiri ubongo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Tume ya Nguvu za Atomiki nchini (TAEC), Peter Ngamilo, kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam, akielezea umuhimu wa kutumia mionzi na athari zake kwa jamii.

“Watu wazima wasitumie simu ikiwa imeisha chaji na akiwa anachaji kwani ina madhara pia endapo itakuwa imeshika moto kwa muda mrefu anaweza kupata matatizo ya kuumwa kichwa,” amesema.

Akizungumzia simu kwa watoto, Ngamilo amesema jamii nyingi hazifahamu athari zake kwani simu hizo mionzi yake ina uwezo wa kuharibu ubongo wa mtoto kwa kuwa haujakomaa.

“Kuna aina mbili za mionzi ya simu, kuna ya minara na ile ya simu lakini ya minara haina madhara ila ya simu endapo atapewa mtoto na kutumia muda mrefu inaharibu ubongo wake hivyo jamii ibadilike katika hili,” amesema Ngamilo.

Hata hivyo, akizungumzia faida za mionzi amesema hutumia katika kilimo, hospitali, viwandani, ujenzi na hata kufanyia tafiti mbalimbali lakini haitakuwa na madhara endapo watumiaji watakuwa na elimu pamoja na leseni za matumizi ya mionzi hiyo kutoka TAEC.

Naye Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi  Teknolojia na Ufundi, William Ole Nasha   akitembelea banda hilo alipongeza hatua za elimu wanazofanya huku akiwashauri katika maonesho ya mwakani wafike na aina mbalimbali za mashine ya mionzi kuonesha mifano yake ili jamii ielewe zaidi kwa kuwa ni muhimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles