26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mwandishi wa Polisi atoa ushahidi kesi ya kina Mbowe

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

SHAHIDI wa sita katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, Koplo Charles, amedai alipoona mihemko ya  wafuasi wa chama hicho, aliamua kukimbilia katika gari la Polisi kunusuru kamera yake.

Koplo Charles alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi, alidai mihemko hiyo ilisababishwa na hamasa aliyoitoa Mbowe kwa kauli ya kuwapandikiza chuki wafuasi hao dhidi ya Serikali.

Alidai Februari 16, 2018 alipangiwa kazi kama mwandishi wa habari kuripoti mkutano wa kufunga kampeni wa Chadema katika viwanja vya Buibui, Kinondoni, Dar es Salaam.

Alidai alijiandaa na vitendea kazi vyake ikiwamo kamera ya kupiga picha za video, ilipofika saa 10 alasiri alifika katika viwanja hivyo kuanza kazi.

“Saa 10 alasiri watu walianza kukusanyika na mshereheshaji alitangaza kwamba viongozi wakuu wa chama wameshafika, baada ya muda wabunge na viongozi wakuu walipanda jukwaani, nilimsikia Mbowe akitoa kauli za kufanya hamasa ya kuichukia Serikali.

“Wanachama walipata hamasa na mihemko iliyosababisha wapate jazba ya kuichukia Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.

“Wananchi waliokuwa wamekaa walinyanyuka na kuhamasika, mimi na waandishi wenzangu tulitawanyika pale tuposimama karibu na jukwaa, nilikimbilia kwenye gari la Polisi kunusuru kamera,” alidai Koplo Charles.

Alidai kuwa alipotoka eneo la tukio, alifika ofisini salama, alikwenda kumpa taarifa RCO, akamwagiza atunze picha za video alizopata kwenye mkutano huo kwa kuwa zitatumika kama kielelezo na kwamba tayari bosi wake huyo alishafungua kesi dhidi ya vigogo wa Chadema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles