27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya Utalii ya Chemchem yatoa baiskeli za Sh milioni 21 kwa walemavu Babati

Mwandishi wetu, Babati

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti amekabidhi baiskeli 31 kwa walemavu zenye thamani ya sh 21 milioni.

Baiskeli hizo zimetolewa na Taasisi ya uhifadhi ya chemchem ambayo imewekeza Utalii wa picha na hoteli Wilayani Babati.

Mkuu wa mkoa Manyara, Joseph Mkirikiti akiwa na Mkurugenzi wa Chem Chem, Nicolas Negri na Mkuu wa wilaya Babati, Lazaro Twange wakikabidhi Baiskeli.

Akizungumza leo Desemba 22, wakati akikabidhi Baiskeli hizo, Mkirikiti alishukuru taasisi ya Chemchem kutoa Msaada huo na kutaka iendelee kusaidia jamii mkoa wa Manyara.

“Tunashukuru kwa Msaada huu lakini isiwe mwisho endeleeni kutoa kama mchango wenu kwa jamii na mimi leo ntatoa mchele kwaajili wa sikukuu kwa walemavu hawa pia fedha kidogo za kuwasaidia,” amesema Mkirikiti.

Mkurugenzi wa chemchem, Nicolas Negri amesema msaada huo ni sehemu ya baiskeli 242 ambazo wanakusudia kutoa kwa walemavu.

“Biashara yetu kubwa sisi ni Utalii hivyo kama tukiendekea kuhifadhi mazingira na kutunza wanyama tutaendelea kupata Watalii na kunufaika wote,” amesema Negri.

Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara ina jumla ya walemavu 1811 wa aina mbalimbali ikiwepo walemavu wa viungo 249.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles