Na Mwandishi Wetu, Pwani
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya ameshauri Watendaji kuanza kutumia taarifa za mfumo wa Anwani za makazi Postikodi kwenye barua za ofisi ili kurahisha mawasiliano kwa watu kujua eneo zinapopatikana Ofisi.
Naibu Katibu Mkuu huyo ameyasma hayo leo Alhamisi Mei 19, 2022 katika ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Kibaha Mji, mkoani Pwani alipofika kujionea utekelezaji wa Operesheni Anwani za makazi.
“Watendaji tuanze kujitambulisha kwenye mikutano kwa mfumo wa Anwani za makazi ili kutoa hamasa zaidi kwa wananchi,” amesema Mmuya.
Upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mkoani A Kibaha, Jakson Mwakalima amesema tayari wameshapata mtengenezaji wa vibao vya nyumba, ambavyo mwananchi anaenda kununua kwa shilingi elfu Mbili na kubandika kwenye nyumba yake.