T-PAIN: MKATABA UNAMPA WAKATI MGUMU

0
660

NEW YORK, MAREKANI


RAPA T-Pain ameweka wazi kuwa anashindwa kuachia nyimbo mara kwa mara kutokana na kubanwa na mkataba wake chini ya lebo ya RCA.

Msanii huyo amesema tayari ana nyimbo nyingi ambazo ameziandaa, lakini kutokana na mkataba wake unavyosema, anashindwa kuwapa burudani mashabiki wake.

“Nimekuwa kimya kwa muda mrefu sana, si kama kazi hazipo hapana, zipo nyingi sana ila mkataba wangu unataka nitoe kazi kwa muda fulani, nimewamisi sana mashabiki zangu.

“Niwaondoe wasiwasi kwamba baada ya miezi sita kuanzia sasa kazi zangu zitaanza kusikika, hivyo mashabiki wakae tayari kwa kunipokea upya,” alisema T-Pain.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here