24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

BEBE COOL: WATOTO SITA HAWANITOSHI

KAMPALA, UGANDA


NYOTA wa muziki nchini Uganda, Bebe Cool, baada ya wiki iliyopita kuthibitisha kuwa amepata mtoto wa sita, sasa amesema watoto hao hawatoshi katika maisha yake.

Msanii huyo ambaye alifanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake, Zuena Kirima, kwa miaka 14 iliyopita, amesema lengo lake ni kuwa na familia kubwa na yenye furaha.

“Nashukuru Mungu kwa kutuongezea ukubwa wa familia yetu, lengo la familia yetu ni kuwa kubwa na tunaamini kwa uwezo wake Mungu tutafanikiwa kama tulivyopanga.

“Kwa sasa nina jumla ya watoto sita, lakini bado hawanitoshi, natamani kuwa na wengi zaidi ya hapo kwa kuwa napenda sana watoto katika maisha yangu, namuomba Mungu aniwezeshe kupata wengine wengi,” alisema Bebe Cool.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles