21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Swahili Fashion Week kutoa ajira kwa vijana

NA JEREMIA ERNEST

KAIMU Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Matiko Saimon, amewapongeza waandaaji wa tamasha la mitindo nchini ‘Swahili Fashion Week’ kwa kutoa ajira kwa vijana kila mwaka.

Tamasha hilo ambalo mwasisi wake ni mbunifu mkongwe Mustapha Hasanali, mwaka huu ni msimu wa 14 , litafanyika kuanzia Desemba 3 – 5,2021 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam,  Saimon, amesema kila mwaka Swahili Fashion Week inatoa ajira zaidi ya 300 kwa vijana jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi.

“Kila mwaka vijana  zaidi ya 300 wanamitindo na wabunifu wa mavazi hupata ajira pamoja na kujitangaza  kupitia jukwaa hili kwa sababu ni moja ya tamasha kubwa la mitindo hapa nchini , napenda kumpongeza Mustapha Hasanali na timu yake na kuwaomba wazidi kuongeza bidii katika kukuza sekta hii,” anasema

Kwa upande  Hasanali, amesema mwaka huu kuna zaidi ya wabunifu 60 wanaoonyesha mavazi yao na tuzo zaidi ya 20, zitatolewa kwa wadau mbalimbali.

“Tupo katika mchakato wa kupigia kura wadau ambao wameingia katika vipengele tofauti kwa ajili ya kuwania tuzo zitakazo tolewa wakati wa tamasha hili, niwaombe wadau kupigia kura wale ambao wamefanya vizuri katika kipindi cha mwaka huu.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles