Sydney, Australia
WATAFITI kutoka Chuo Kikuu cha Queensland and Monash, walisafiri hadi kisiwa cha Fraser, Australia kuwawinda na kuwashika buibui hatari wa nchi hiyo.
Watafiti hao wanasema kuwa protini iliyopo katika sumu ya buibui inaweza kusaidia kulinda ubongo kutokana na jeraha baada ya kiharusi.
Inaelezwa kuwa wanasanyasi waligundua kwamba tiba ya protini hiyo ilifanya kazi ilipotumiwa katika panya wa maabara.
Wanasema ilionyesha kwamba inaweza kuwa tiba nzuri katika siku zijazoi lakini haijajaribiwa miongoni mwa binadamu.