23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Sumaye akemea rushwa, ubinafsi

sumayeNA MWANDISHI WETU, Dar es Salaam
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amesema lawama zinazotolewa na wananchi nchini zinatokana na kukithiri kwa rushwa, ufisadi, ubinafsi na uwepo wa biashara za dawa za kulevya hapa nchini.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana, wakati wa maadhimisho ya siku ya kazi ya Chuo cha Ustawi wa Jamii (IST).

“Binadamu wenye uzalendo na maadili mema wanawajali wenzao na hawawezi kuangamiza maisha ya wengine, wakiwamo vijana kwa kufanya biashara ya dawa za kulevya kwa sababu tu wanatafuta utajiri.
“Leo watu wanashindana kwa sayansi na teknolojia na mataifa yanafanya utafiti wa kukaa katika sayari nyingine, lakini kwetu sisi kuna watu wanakata viungo vya vijana wenye ulemavu wa ngozi kwa sababu tu wanatafuta utajiri.
“Hayo ni matunda ya kukosa elimu, maadili na ubinafsi uliopitiliza kwa sababu binadamu mwenye maadili mema hawezi kufanya hayo.
“Binadamu huyo hawezi kuua na hawezi kuiba fedha za umma zilizotakiwa kujenga miradi ya kusaidia jamii, kama kununulia dawa, kujenga shule, kujenga barabara, kuweka maji na kuweka umeme.

“Kama hali hii haitadhibitiwa, itapanda mbegu ya chuki na mapambano kati ya wenye nacho na wasio nacho, itapanda mbegu kati ya wanaoongoza na wanaoongozwa na itapanda pia mbegu kati ya wenyeji na wageni,” alisema Sumaye.

Alisema dawa ya uhakika ya matatizo hayo ni kuwa wazalendo wa kweli na kuwa watumishi wema wa umma, badala ya kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi binafsi.

Akizungumzia nafasi ya vijana katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, alisema uchaguzi ni tendo muhimu katika kutekeleza demokrasia na ni hitaji linalotambuliwa kikatiba.

“Sote tunajua uchaguzi huingiza madarakani Serikali mpya itakayotuongoza kwa miaka mitano ijayo.

“Tunajua endapo uchaguzi hautafanyika kwa haki na uwazi, unaweza ukasababisha machafuko nchini na nchi nyingi, hasa Afrika zimeingia katika machafuko kwa sababu ya dhuluma katika uchaguzi.
“Katika hili, leo nataka nizungumzie zaidi ni nini wajibu wa vijana, hasa ninyi wasomi katika uchaguzi huu au uchaguzi mwingine wowote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles