27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Statoil yataja walioingia tano bora mashujaa wa kesho

StatoilNA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Statoil Tanzania imetangaza majina ya vijana watano walioingia fainali za shindano la biashara la mashujaa wa kesho lenye lengo la kuhamasisha ujasiriamali kwa mikoa ya Kusini mwa Tanzania yaani Mtwara na Lindi.

Meneja wa shindano hilo, Erick Mchome, amewataja washindi hao kuwa ni Razaki Kaondo, Edward Timamu na Sifael Nkiliye (walioshiriki timu moja), Saleh Kisunga, Azizi Doa na Yunus Mtopa.

Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi kuwasilisha mawazo yao ya biashara ambayo baadaye yalibadilishwa na kuwekwa kwenye andiko la biashara.

Mwaka huu shindano hili lilivutia vijana zaidi ya 400 waliowasilisha mawazo ya biashara zao zinazolenga sekta mbalimbali za uchumi kama kilimo, ufugaji, mawasiliano na biashara nyingine ndogondogo. Vijana waliruhusiwa kushiriki mmoja mmoja au hata kuunda vikundi vya watu wawili mpaka watatu.

Mshindi wa shindano hili atatangazwa Ijumaa 15 Aprili jijini Dar es Salaam katika hafla maalumu iliyoandaliwa na Statoil ili kumpongeza mshindi huyo na wenzake wanne waliofanikiwa kuingia fainali. Mshindi huyo atajinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 5,000 wakati washindi wanne waliobakia watapata dola 1,500 kila mmoja. Washindi wengine watano waliofanikiwa kuingia kumi bora watapata dola 1,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles