22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mourinho akanusha kumalizana na Man United

MourinhoMANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa zamani wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, ameweka wazi kwamba hadi sasa hajasaini mkataba wowote na klabu ya Manchester United, lakini mwishoni mwa msimu huu ataweka wazi klabu ya kuitumikia.

Ilidaiwa kwamba kocha huyo tayari amesaini mkataba wa awali, lakini amedai kuwa bado ila lazima apate timu ya kuitumikia katika msimu mpya hata kama sio Manchester United.

“Van Gaal ni rafiki yangu wa karibu sana, niliwahi kufanya naye kazi kwa miaka kadhaa, nimekuwa nikihusishwa kurudi uwanjani, ni kweli wakati wa majira ya joto lazima nitakuwa na timu ila niweke wazi kwamba hadi sasa sijasaini mkataba wowote na Man United au klabu yoyote.

“Kutokana na hali hiyo naweza kusema kwamba nakaribisha ofa kutoka klabu yoyote au timu ya Taifa ambayo itakuwa tayari kufanya kazi na mimi,” alisema Mourinho.

Hata hivyo, kocha huyo amesema kwamba japo kuna klabu nyingi ambazo zinamuhitaji lakini lengo lake ni kuzifundisha klabu za Ligi Kuu nchini England.

“Niweke wazi kamba napenda kufundisha klabu, lakini nitakuwa na furaha kama nitapata nafasi ya kufundisha klabu za nchini England, naipenda nchi yangu lakini napenda Ligi ya England.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles