23.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Pacquiao amaliza pambano la mwisho

1LAS VEGAS, MAREKANI

BONDIA Manny Pacquiao, tayari amemaliza pambano lake la mwisho na kutwaa ubingwa dhidi ya mpinzani wake, Timothy Bradley, juzi kwenye ukumbi wa MGM Grand Arena, nchini Marekani.

Mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwa Pacquiao ambaye alitangaza kustaafu baada ya kumalizika kwa pambano hilo.

Katika pambano hilo, Pacquiao alifanikiwa kumwangusha mpinzani wake mara mbili kutokana na ngumi nzito kwenye mchezo huo wa Welterweight.

Pacquiao alitangazwa bingwa kutokana na pointi zilizotajwa na majaji watatu, ambapo alishinda kwa 116 dhidi ya 110 za mpinzani wake.

“Ni furaha kubwa kutwaa ubingwa huu, kilichobaki sasa ni kurudi nyumbani kwa ajili ya kuisaidia familia yangu na wananchi wa Ufilipino, ninachokifikiria sasa ni juu ya kustaafu ngumi.

Bradley naye alisema kwamba, uwezo wake ulikuwa mdogo wa kuweza kumpiga Pacquiao, hivyo anatakiwa kufanya mazoezi ya nguvu kuweza kufikia hatua ya mpinzani wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles