28.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

Mtoto wa B.I.G amjia juu P. Diddy

p-diddy-65th-cannes-film-festival-01NA BADI MCHOMOLO

BAADA ya msanii wa hip hop nchini Marekani, Sean Combs ‘P. Diddy’, kusema kwamba anatarajia kuandaa tamasha la kumkumbuka marehemu, Notorious B.I.G, mtoto wa marehemu amemjia juu msanii huyo.

Diddy alisema kwamba atafanya tamasha Mei 20 mwaka huu kwa ajili ya kumkumbuka B.I.G, lakini mtoto wa B.I.G, T’yanna Wallace, amedai kwamba tamasha hilo halina maana kwa kuwa Diddy hajawahi kuisaidia familia ya marehemu.

“Sioni sababu ya P. Diddy kufanya tamasha hilo ambalo anajitafutia fedha, tangu baba yangu amefariki sijawahi kuona msaada wake wowote katika familia hii.

“Sasa ameandaa tamasha hata tiketi hajatoa katika familia yetu, hii itakuwa ni siku ya Bad Boy na sio ya kumkumbuka baba yangu,” aliandika kwenye akaunti ya Twitter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles