23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Stand yashtukia janja ya TFF

katibu+yangaNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

KLABU ya soka ya Stand United imesema kitendo cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  kusimamisha  uchaguzi wa klabu hiyo ni mbinu ya kutaka kuhujumu uchaguzi  wao  uliotarajiwa kufanyika  Juni 24 hadi Julai 3 mwaka huu.

TFF ilifikia uamuzi huo  baada ya kutokea msuguano kati  ya makundi mawili  ndani ya klabu hiyo, ambayo ni Stand United  Kampuni na Stand United Wanachama  yaliyotaka  kufanya  uchaguzi wa viongozi wapya.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Dk. Jonas Tiboroha, alisema hakukuwa na sababu  za msingi za kusimamisha uchaguzi huo kwa kuwa  kati ya makundi hayo mawili, moja lipo kisheria na linatambulika na klabu kwa kuwa  ni wanachama halali.

“Kundi la Stand Kampuni lenye  watu 52 ndio wanachama halali wa klabu hii lilisajiliwa  mwaka jana, lakini hao wanaojiita Stand United wanachama  si wanachama halali wa klabu hii kinachotokea sasa wanatumika kuhujumu uchaguzi huu.

“TFF inajaribu kuingilia kati uchaguzi huu, kwa kuwa kuna watu  wao  ambao  wana masilahi nao wanataka waingie  ndani ya klabu hii  ili kuivuruga,  lakini jambo hilo halitawezekana,” alisema Tiboroha.

Hata hivyo, Tiboroha alisema kutokana na TFF kuvunja sheria mara kwa mara waliamua suala hilo kulifikisha Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ili kupata mwafaka na kuendelea na mchakato wao wa uchaguzi.

“Stand hakuna tatizo hata kidogo kwa kuwa kila kitu kipo wazi, TFF inachofanya ni kupindisha sheria na kanuni ambazo tumekuwa  tukizitunga  wenyewe ili  zituongoze.

“Kuna kesi nyingi za malalamiko juu ya vitendo vya  uvunjwaji wa sheria vinavyofanywa na TFF kutoka  mkoa wa Tabora, Kigoma na Geita,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles