26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Kimenya ataka milioni 40/- Simba

Salum KimenyaNA ZAITUNI KIBWANA

BEKI wa kati wa Tanzania Prisons, Salum Kimenya, amesema anahitaji Sh milioni 40 ili aweze kumwaga wino kwenye kikosi cha Wekundu wa Msimbazi, Simba.

Kimenya ambaye amekuwa kwenye kipindi cha mafanikio msimu uliopita, amesema hakuna kinachomkwamisha kutua kwenye klabu hiyo zaidi ya fedha anayoitaka.

Alisema dau dogo ambalo amekuwa akitajiwa na viongozi hao wa Simba, ndilo limekuwa kikwazo cha yeye kutua kwenye klabu hiyo.

“Simba mwaka jana walinitaka wakataka kunipa milioni 30 nikakataa nikawaambia nipeni 45 dili likavunjika na safari hii nawashangaa kabisa dau lao eti wanataka kunipa Sh milioni 20, nimewaambia wanipe 50 pia imekuwa ni kuomba wapunguziwe sasa imefika 40 hapo siwezi kupunguza tena,” alisema.

Kimenya alisema amewapa muda viongozi hao wa Simba mwisho wiki hii, ikifika Jumatatu ijayo basi atatia saini kwenye klabu yake ya Prisons.

“Nawapa mpaka wiki hii iwe mwisho kama wakikaa kimya basi nitasajili kwenye klabu yangu ya Prisons ambayo nimemaliza nayo mkataba,” alisema.

Simba inasuka upya kikosi hicho msimu ujao ambapo mpaka sasa tayari imewasajili nyota watano ambao ni mabeki; Emmanuel Semwanza, kiungo Muzamil Yasir, Mohammed  Ibrahim, Hamad Juma na mshambuliaji, Jamal Mnyate.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles