25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Stafeli husaidia kupunguza makali ya dawa za saratani

soursop

Na MWANDISHI WETU,

MATUNDA ni muhimu katika mwili wa binadamu, japo watu wengi huwa hawayatilii maanani.

Utakuta mtu anamaliza miezi miwili hadi mitatu hajala tunda lolote.

Wengi husubiri mpaka apate ushauri kutoka kwa daktari pindi anapokuwa mgonjwa, ndio maana hukumbwa na matatizo mengi bila ya wao kujijua.

Safu hii imekuwa ikiwaletea umuhimu wa matunda mbalimbali na mbegu zake ili angalau kila mmoja aweze kujijengea utamaduni wa kula matunda mbalimbali kila siku.

Matunda ni afya na pia ni tiba ya maradhi mbalimbali. Leo tutazungumzia faida za tunda la stafeli ambalo wengi hulidharau lakini linafaida nyingi mwilini.

Faida za stafeli

Majani yake hutumika kama chai. Pia hutibu maradhi mbalimbali kama vile kuharisha damu, mafua na husaidia mfumo wa umeng’enyaji wa chakula.
Mizizi yake huua minyoo wa aina mbalimbali, wakati mbegu zake hutengenezwa dawa na kufukuza wadudu waharibifu.

Tunda hili ni chanzo kikuu cha  vitamin C, madini ya chuma na asilimia 12 ya stafeli ni sukari salama.
Juisi ya stafeli inaweza kuwa chakula tosha na chenye virutubishi ingi mwilini.

Aidha, wagonjwa kama wa saratani mara nyingi wanapokuwa kwenye tiba, madaktari huwashauri pia kula tunda hili ili kumpunguzia mgonjwa makali ya dawa na kupunguza maumivu.

Hii ni kwa sababu maumivu ya saratani ni makali mno hivyo wagonjwa hupewa dawa kali  za maumivu. Hivyo, matumizi ya tunda hili humpunguzia mgonjwa kuepuka madhara ya dawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles