25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Soko kubwa duniani la viungo vya binadamu hili hapa

Baadhi ya vijana waliouza figo zao wakionesha alama zilizotokana na operesheni.
Baadhi ya vijana waliouza figo zao wakionesha alama zilizotokana na operesheni.

MIAKA mitatu iliyopita, Vikas (si jina lake halisi) alilazimika kuacha shule ili kumsaidia baba yake kulima katika shamba la familia karibu na mji wa kaskazini mwa India wa Kanpur, licha ya kwamba ni kazi ambayo aliichukia.

Lakini leo hii amebadili kazi. Kijana huyo mwenye umri wa miaka miaka 26 anajipatia kipato akiwa kama mmoja wa mamia ya mawakala wa figo waliotapakaa nchi nzima, kitendo kilichochewa na ongezeko la soko jeusi la viungo vya binadamu vinavyotafutwa zaidi duniani lenye thamani ya mamilioni ya dola.

“Iwapo una fedha na unataka haraka, unakuja hapa. Nitakutafutia mtoaji na unaweza kwenda nyumbani ukiwa na figo mpya ndani ya mwezi,” alisema kwa masharti ya kutotajwa jinale halisi.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Asia Kusini kwa sasa inaongoza duniani kama kitovu cha utalii wa upandikizaji viungo vya binadamu, huku India ikiwa miongoni mwa wasafirishaji wakubwa zaidi wa figo. Kila mwaka raia zaidi ya 2,000 wa India huuza figo zao huku nyingi zikienda kwa wageni.

Wakala mwingine Aadarsh, mwenye makazi yake Mumbai, ambaye pia aliomba kuhifadhiwa jinale kwa hofu ya kibano cha polisi, alisema ‘figo zake’ zinaenda kwa wanunuzi kutoka Canada, Israel, Uingereza, Saudi Arabia, Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain, ijapokuwa wanunuzi wengi kwa sasa hutokea ndani ya India.

Ongezeko ya maradhi ya figo, kisukari na shinikizo la juu la damu kumesababisha ongezeko la mahitaji ya figo duniani, ambayo yanapiku usambazaji.

Kupigwa marufuku kimataifa kwa mauzo ya viungo vya binadamyu, sambamba na kusita kwa tamaduni nyingi kuchangia figo ikiwamo baada ya kifo kwa ajili ya ndugu zao kama sheria za nchi nyingi zinavyotaka, kunamaanisha kuwa wagonjwa mara nyingi hulazimika kutegemeza uhai wao kwa mashine maalumu kwa miaka mingi, hadi pale watakapopata mtoaji aliye tayari.

Kwa sababu hiyo, pengo baina ya mahitaji na usambazaji halali wa figo limezibwa na soko kubwa kabisa duniani la siri la viungo vya binadamu, ambalo limejikita zaidi nchi za India, Nepal, Bangladesh, Pakistan, Sri Lanka na Iran.

Hata hivyo, katika miaka ya karibun mji mkuu wa Sri Lanka, Colombo umekuwa makao makuu ya mtandao huo mpana huku operesheni nyingi za upandikizaji zikifanyika hapo na kuvutia wanunuzi wa viungo kutoka mbali hadi Israel na Marekani.

Kupanda kwa Colombo kumetokana na India kupitisha sheria kali kuhusu biashara hii mwaka 2008 baada ya kukamatwa kwa kinara wa figo, aliyekuwa akiendesha moja ya magenge makubwa kabisa ya usafirishaji figo duniani.

Wahisani wengi pia hutoka Iran, nchi pekee duniani ambako uuzaji figo ni halali ijapokuwa si kwa wageni.

Figo hugharimu kuanzia dola 53,000 sawa na Sh milioni 108 hadi  milioni 234 za Tanzania ikihusisha kila kitu kuanzia bili za hospitali, ada ya daktari, malipo kwa mtopaji, gharama zake za safari na malazi na mwisho kamisheni kwa wakala.

Ijapokuwa biashara hiyo haramu imekuwa ikishamiri tangu miaka ya 1990, mawakala kama Vikas na Aadarsh hutumia mtandao wa Facebook  wakiieleza kama makundi yanayosaidia upandikizaji wa figo na viungo vingine.

Mara hitaji la figo fulani linapowasilishwa kwa wakala, kinachofuata ni kuweka mtandaoni taarifa ya hitaji, ikiahidi donge nono kwa figo nzuri yenye afya.

Ujumbe mara nyingi hujieleza kwa namna ya masikitiko ya uwapo wa ‘ndugu aliye karibu na kifo,’ ambaye anatafuta mhisani mwenye damu mfanano kwa haraka.

Lakini uendeshaji shughuli katika mitandao ya juu una vizingiti vya sheria. Kwa sababu hiyo Vikas hutengeneza majina mapya bandia kila baada ya wiki tano au sita na kuachana na namba zote za simu alizotumia.

“Nakwepa kuonana na yeyote hadi ninapokuwa na uhakika kwamba si mtego. Pia, kamwe sijibu simu za watu ambao nilishakutana nao huko nyuma. Ukikutana na kufanya biashara nami usitarajie kuniona tena mwezi ujao, anaeleza Vikas.

Alisema huwalenga zaidi watoaji wa figo vijana wasiovuta sigara walio katika umri wa miaka 20 au ya awali ya 30 hasa wanaume, kwa vile hao ni rahisi kusafiri wenyewe ng’ambo. Wale ambao tayari wana hati za kusafiria wanapewa kipaumbele zaidi.

Mara imani inapojengeka, mtoaji mtarajiwa hupelekwa kuchukua vipimo vya damu na tishu katika maabara zilizpo mjini New Delhi na Uttar Pradesh.

Wale waliopo kusini magharibi mwa nchi kwa kawaida hupelekwa klatika hospitali kubwa na binafsi iliyopo Chennai na baadhi ya madaktari ni sehemu ya mtandao wa Colombo, na husaidia kuharakisha mchakato.

“Maabara hunitumia ripoti za vipimo, lakini kwa wakati mwingine hutuma moja kwa moja kwa madaktari Colombo. Mtu fulani aliyepo Chennai hulipia vipimo hivyo. Iwapo vipimo vinakubalika, nafanya mpango mara moja kumsafirisha mtoaji figo kwenda Colombo,” alisema Vikas.

“Tayari nakuwa na nyaraka zote ikiwamo hati za kusafiri zinazotakiwa na nina mawasiliano za mhusika wa kumpokea ndani ya siku zijazo.”

Vikas mara nyingi huhitaji kuwasindikiza wauzaji hadi Mumbai. Kwa kawaida hupanga kuonana nao wakati mwingine kwa mara ya kwanza katika stesteni ya reli ya New Delh, ambako huchukua treni hadi Mumbai. Hiyo ni kwa wale watoaji figo wanaotokea familia masikini, wasio na elimu au mwamko, ambao husita kusafiri peke yao,” anasema.

“Huagizwa kuwaacha katika hoteli au nyumba ya wageni katika mahali palipopangwa. Fedha yangu kwa kawaida huikuta mapokezi. Wakati mwingine nawaacha katika maduka ya simu na kuondoka bila kuangalia nyuma, kwa mujibu ya maagizo.

Nachukua kamisheni yangu na kamwe simuoni tena mtoa figo. Mtoa figo huenda Colombo na wakala mwingine kwa ajili ya operesheni,” Vikas anasema.

Mtoa figo wake wa kwanza alimpatia kamisheni ya rupia 25,000 sawa na Sh 800,000 miaka mitatu iliyopita.

Lakini sasa anatengeneza rupia 50,000 hadi 80,000 sawa na Sh milioni 1.5 hadi sh milioni mbili kwa kila mtoaji figo. Mwaka jana alitengeneza dili lililompatia rupia zaidi ya nusu milioni moja sawa na Sh milioni 15.

Kwa mujibu wa mawakala hao, watoaji figo, ambao wana hati za kusafiria hulipwa rupia 400,000 sawa na Sh milioni 13, ambazo hulipwa siku mbili kabla ya operesheni. Iwapo hati za kusafiria huandaliwa na mawakala, watoa figo hupokea rupia 300,000 sawa na Sh milioni 10.

Watoa figo na mawakala hukaa katika makazi ya kifahari mjini Colombo, kilomita moja tu kutoka zilipo hospitali tatu ambazo huhudumia wateja wa kigeni. Wahisani kwa kawaida hurudi nyumbani baada ya siku 18-25.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles