23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Spika Ndugai, Masele hapatoshi

NA AZIZA MASOUD,DAR ES SALAAM

SPIKA wa Bunge Job Ndugai  amesema suala la kumuita Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Afrika(PAP) Steven Masele  katika Kamati ya Maadili lipo katika mamlaka ya kiti chake hivyo hakuwa na sababu ya kujadiliana na wabunge wengine.

Kauli ya Spika Ndugai imekuja wakati  juzi   kukiwa na malalamiko ya wabunge juu ya mamlaka  ya spika kumuita mbunge huyo ambaye uteuzi wake ulishirikisha  bunge zima.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC  Idhaa ya  Kiswahili  ambapo mwandishi  alimuuliza kama kabla ya kumuita kwenye kikao   aliwashirikisha  watu waliomteua.

“Suala hilo lipo katika mamlaka ya spika,kumuita mtu ni kumpa haki ya yakusilizwa hivyo watu wanapaswa waelewe vizuri kwa sababu wahusika  wanaweza wakachukua  hatua  za kinidhamu lakini bado wananchi wakawauliza  kama tulimisikiliza na ili mtu umsikilize lazima aitwe,kwa hiyo kuitwa  ni jambo la  kawaida na ni kwa mamlaka ya spika.

“Atafika hapa atakwenda kukutana na wabunge wenziye ambao watamuuliza maswali yatakayokuwapo  na yeye atapata haki ya kujielezea ndani ya bunge si nje,kama haki ni ya kwako ivi kwa nini wenzako wakuonee, ”alisema Ndugai.

Alisema hawajakurupuka kumuita mbunge huyo  kwakuwa ameitwa kwa mambo ya hapa nyumbani ambayo yanahusisha utovu wa nidhamu  na si hayo yanayoendelea katika bunge la Afrika.

“Yeye anaunganisha hilo na matendo ambayo anayafanya  ambayo pia yanatudhalilisha kama nchi,lakini hatujamuita   kwa mambo ya Afrika Kusini  sisi tumemuita kwa mambo ya hapa nyumbani ya utovu mkubwa wa nidhamu,watanzania watulie baada ya muda  suala hilo litaletwa bungeni  wataelezwa anatuhumiwa nini na majibu yake yalikuwa ni nini kwa sababu lazima liletwe bungeni hilo suala,”alisema Ndugai.

Alisema  kiutaratibu  mbunge unapopata wito wa kwenda katika kamati ya maadili  anapaswa kuupa kipaumbele kwakuwa muhimili wenye nguvu kisheria

“Unapopata wito kwa kawaida wa kwenda kwenye kamati ya maadili ya bunge  ambao ni  muhimili wenye nguvu kisheria unapaswa kuacha chochote unachokifanya  ili  uupe wito huo kipaumbele  cha hali ya juu.

“Na Masele  mpaka hivi sasa hajaitikia wito huo ambao  tunahesabu kama ukaidi anapaswa harudi haraka ili aweze kufika kwenye kamati hiyo kwa ajili ya kujibu tuhuma zilizopo dhidi yake,”alisema Ndugai.

Alipoulizwa kwamba anadhani kwa nini amekaidi amri yake Ndugai alijibu kuwa kudhani kwamba  mbunge huyo amekaidi amri hiyo si sawa.

“Nikidhania itakuwa sio sawa sawa  tumsubiri aje na  atajieleza kule kwa nini amekaidi,”alisema Ndugai.

Alipoulizwa  kuhusu tetesi ya kwamba serikali ilimwamuru Masele aendelee na kazi zake nchini Afrika Kusini  taarifa ambayo inakinzana na amri yake alisema  hawezi kuisemea serikali.

“Mimi siisemei serikali kama kweli serikali imemwambia kwamba yeye akaidi wito wa spika basi kwenye kamati  ya maadili ataeleza hilo,lakini jambo kama hilo  uwezekano wake ni mdogo sana kwa kweli kwa ujumla wake  halipo na ni moja ya sababu kwa nini tunamwita ,huyu ni  kiongozi ambaye ana mapungufu yakinidhamu  anaweza  kusema uongo ambao hata mtu mwingine wa kawaida huwezi kufanya ,”alisema Ndugai.

Alipoulizwa endapo mbunge huyo atakaidi wito wake wa kuja Tanzania  alisema  asingeweza kukaidi zaidi  kwa sababu lazima arudi Tanzania.

“Hawezi kukaidi  zaidi kwa sababu ni lazima arudi Tanzania  labda aamue kuwa  mkimbizi na akirudi Tanzania lazima  afike kwenye kamati ya maadili huu ni wito wa kisheria kama ilivyo wito mwingine wa mahakamani,tunachomuitia hapa ni tabia yake  ya  uchonganishi na ugonganishi  kwa viongozi.

Alipotakiwa kutoa mfano wa tabia za uchinganishi anazozifanya mbunge huyo Ndugai alisema,“hatuwezi kuingia uko lazima kwanza aende kwenye kamati atakapotoka ndo mtaona fitina yenyewe ikoje ambayo ni kama kukosa sifa kubwa sana kwa kiongozi yeyote yule,”.

Wakati Ndugai akitoa ufafanuzi huo juzi  Masele  siku aliongea na chombo kimoja cha habari na kudai kuwa hajamuelewa kiongozi huyo hasa kwa  hatua yake ya kusitisha uwakilishi wake huku akimtuhumu kwa  ukosefu wa nidhamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles