30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kenya yasaini makubaliano na Afrika Kusini kufundisha Kiswahili

Serikali za Kenya na Afrika kusini zimekubaliana kutia sahihi katika Hati ya makubaliano (MoU) ambayo yataweka msingi wa kuanza kufundisha somo la Kiswahili katika mfumo wa elimu wa Afrika kusini

Waziri wa Elimu George Magoha  namesaini Hati ya makubaliano kwa niaba ya serikali ya Kenya, wakati waziri wa elimu ya msingi Mrs.Angelina Matsie Motshekga amesaini kwa niaba ya serikali ya Afrika kuisni.

Makubaliano hayo pia yataipatia serikali ya Kenya nafasi ya kutoa mafunzo ya kiufundi katika sekta ya elimu, mbali ya kupanua wigo na kuongeza matumiza ya Lugha ya Kiswahili kama miongoni mwa lugha rasmi nchini Afrika kusini.

Waziri Magoha amesema MoU hiyo itakuwa kichocheo cha uhusiano kati ya Kenya na Afrika kusini, na kuongeza kuwa lugha ya Kiswahili itakuwa nyenzo imara ya kuunganisha wananchi wa nchi hizo mbili.

Amesema, Wakenya wengi wamefundishwa nidhamu na utaalamu wa afya katika vyuo vikuu vya Afrika kusini, hivyo kubadilishana wataalamu yanazinufaisha nchi zote mbili.

Naye Waziri Motshekga amesema takribani asilimia 40 ya wanafunzi nchini Afrika kusini wanasoma somo la Lugha ya Kiswahili.

Amesema MoU hiyo itawezesha wanafunzi wa Afrika kusini kuchagua kusoma somo la Kiswahili badala ya Lugha za Kifaransa na Kireno.

Lugha ya Kiswahili ni kibantu na ya kwanza kuzungumzwa na wabantu. Ni miongoni mwa lugha inayozungumzwa zaidi katika Nchi za Maziwa Makuu na sehemu ya mashariki na kusini-mashariki mwa Afrika, ikiwemo nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi,Msumbiji, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Inakadiriwa kuwa watu milioni 100 wanazungumza Lugha ya Kiswahili katika maeneo hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles