25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Spika Ndugai amwomba radhi Rais Samia

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amemwomba radhi Rais Samia Suluhu Hassan endapo alihisiwa kutoa neno la kumvunja moyo kutokana na taarifa mbalimbali ambazo zilitolewa katika mitandao ya kijamii kuhusu matumizi ya mkopo wa Sh Trilioni 1.3 zilitolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia amewahakikishia Watanzania yeye ni yule yule ni uimara wake upo palepale na wale waliomrushia matusi amewasamehe bure na wengine hawajui wayatendayo na ndio maana amebeba matusi yote hivyo amedai amekosa na asamehewe.

Spika Ndugai ameomba radhi leo Januari 3,2021 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo amesema amesema kuwa hotuba yake haikuwa na jambo la kukashifu wala kudharau juhudi za Serikali bali alikuwa anasisitiza ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali.

“Kwa hiyo binafsi yangu popote pale ambapo nilihisiwa kwamba nimetoa neno la kumvunja moyo Rais wetu na akavunjika moyo, ninatumia fursa hii kupitia kwenu kumuomba radhi sana mheshimiwa rais na kwa Watanzania wote,”amesema Ndugai.

Spika Ndugai amesema wao ni kitu kimoja na katu haitatokea wakatengana na wataendelea kumsaidia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Katika hali kama hii haiwezi kutokea na haitatokea na si rahisi jambo kama hili kutokea peke yake hataweza, tumsaidie kwa sababu kwa pamoja ndio tutaweza.Mtawasikia Wabunge wapo na Rais na sisi wote tunatekeleza sera ya ilani ya CCM hatugombani  hata siku moja hao washindwe na walegee,”amesema Ndugai.

Pia, amesema nchi nzima inafurahia kwa jinsi mpango wa fedha za Uviko-19 zilivyotumika ambapo ametoa wito matumizi ya fedha hizo yaendelee kutumika hivyo hivyo kwani itakuwa ni faida kwa nchi.

“Mfano kwangu Kongwa nimefuatilia kila chumba cha madarasa kinachojengwa hakuna jengo zuri kama majengo hayo.Tumepiga tiles madarasa yetu yote, tumejenga vyumba 150 wastani wa Sh bilioni 3 Kongwa, makusanyo yetu Halmashauri ya Kongwa ni Sh bilioni 3.

“Nitakuwa mtu wa kubeba dhambi kubwa sana kwa mafanikio makubwa haya  kumpinga Rais,tusimvunje moyo rais wetu mtamsikia kila mbunge na fedha hizi ziliidhinishwa.

 “Wakati naumwa yalijitokeza mambo mbalimbali lakini sikuweza kujibu,tarehe 26,12,2021 nilialikwa na kikundi cha wanadodoma lengo la kikundi hicho ni tushikamane siku moja tujenge kituo utamaduni (Makumbusho),” amesema Ndugai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles