24.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 15, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yahitimisha promosheni ya Bonge la Mpango nawashindi 32

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampeni ya Benki ya NMB ya kuwahamasisha wateja wake kuweka akiba ya Bonge la Mpango Awamu ya Pili ilifungwa rasmi wiki iliyopita kwa washindi 32 kujinyakulia zawadi zenye thamani ya Sh milioni 100.

Miongoni mwa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni hiyo kabambe walikuwa ni wateja 22 wa NMB walioshinda pikipiki za miguu mitatu aina ya Skymark ambazo bei ya kila moja ni Sh milioni 4.5.

Pia katika kuhitimisha shindano hilo la wiki 12 lililoanza mwezi Oktoba mwaka jana washindi 10 walishinda Sh 100,000 kila mmoja. 

Akizungumza jana wakati wa droo ya mwisho iliyofanyika kwenye Tawi la NMB la Bagamoyo mkoani Pwani, Afisa Uhusiano Amana za Wateja wa benki hiyo, Monica Job, alisema kampeni hiyo imefanyika kwa mafanikio na ufanisi mkubwa.

Aidha, kiongozi huyo alitabainisha kuwa promosheni hiyo imenufaisha wateja zaidi ya 170 na kuwachagiza wengine kuchangamkia fursa kama hizo na huduma zinazoendelea kubuniwa na kutolewa na Benki ya NMB.

Lengo la “Bonge la Mpango II” kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake ilikuwa kurejesha fadhila kwa wateja waaminifu na kuwahamasisha kujenga utamaduni wa kuweka akiba.

Kwenye droo ya mwisho iliyosimamiwa na Afisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Pendo Mfuru, washindi 17 walitwaa pikipiki za fainali, watatu wakijibebea pikipiki za mwisho wa mwezi na wawili walishinda pikipiki za droo ya wiki.

“Hii imekuwa ni kampeni iliyofanyika kwa mafanikio makubwa, huku ikiwanufaisha wateja wetu wengi sana. Tuliitumia sio tu kuhamasisha utamaduni chanya wakuweka akiba, bali pia kama sehemu ya utamaduni wa NMB wa kugawana faida na wateja wake na kurudisha kwa jamii. Tunashukuru kwa sababu malengo haya yote yamefanikiwa kwa asilimia kubwa,” alisema Job.

Kwa upande wake, Mfuru aliipongeza NMB kwakampeni hiyo akisema kuwa ilifanyika kwa kufuata sheria, vigezo, masharti na taratibu zinazosisitizwa na GBT na kwamba benki hiyo ilizingatia hayo yote katika kila droo ya Bonge la Mpango II.

Katika promosheni hiyo, kila wiki washindi 10 walijishindia pesa taslimu na wawili pikipiki za Skymark, huku droo za mwisho wa mwezi zikiwazawadia washindi watatu pikipiki hizo za kisasa. 

Jumla ya Skymark 50 zilinyakuliwa kwenye kampenihiyo iliyokuwa na zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 246 ambazo washindi wake walitoka sehemu mbalimbali nchini.

Washindi walioshinda pikipiki za droo ya mwezi Desemba na matawi yao kwenye mabano ni: Emmanuel Kavishe (Zanzibar), Mbila Salum (Mafinga) na Albert Mhehe (Mkwawa).

Waliojinyakulia pikipiki 17 za droo ya fainali ni: Frank Mgeni (Ngaramtoni), Bundala Gwanona (Geita), Mary Martine (Kenyatta Road), Misoji Joseph (Kenyatta Road), Martha Makorere (Tarime), Ambakisye Kyomo(Kaitaba), Paschal Kaloli (Geita) na  Herieth Alphonce (Babati).

Wengine ni Elineema Ezekiel (Babati), Khamis Abbas (Sikonge), Hamalos Kahindi (Nzega), Mathias Lusendamila (Manonga), Clement William (Wami), Michael Kabume (Mvomero), Glory Mwalongo (Mvomero), Marc Constantine (Wami) na Aziza Nzoto (Mvomero).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles