Brighiter Masaki, Dar es salaam
SHIRIKA la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Serikali ya mtaa wa Vikongoro wamejitolea kuchangisha fedha ya kujenga ukuta shule za msingi zilizopo chanika jijini dar es salaam wakianza na shule ya Singizio na shule ya msingi Chanika.
Akizungumza na MTANZANIA, Afisa Mradi wa SOS, Godwin Mzirai, alisema kuwa viongozi na wananchini kwa ujumla wanawajibu wa kushiriki katika maendeleo ya jamii maana ni jukumu la watu wote.
Anasema kuwa SOS imejikita katika Miradi mitatu ambayo ni Mradi wa mafunzo kwa walimu ili kutumia adhabu mbadala, mradi wa Cheza na jifunze unao hamasisha wanafunzi kujifunza matumizi ya barabara pamoja na
“Kuchangia maendelea katika jamii ni jukumu la watu wote kwa kuwa hali ya wanafunzi mashuleni hususa katika shule za Chanika, sio nzuri wanahitaji msaada wa hali na mali kwa kuwa wanasoma kwa shida na shule hazina uzio hali inayopelekea kufanyiwa vitendo vya ukatili,”anasema Mzira.
Kwa upande wake Afisa Usiano na elimu kwa uma, Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu anasema kuwa kitendo cha ukatili kwa watoto ni jambo la kusikitisha hivyo alichangia mifuko 100 kusaidia ujenzi wa shule hiyo.