27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Mwakifamba: Mkutano wa ndani CCM Bashiru, Samia Suluhu na Makonda wahusika


Brighiter Masaki, Dar es salaam

KATIBU Mwenezi Ccm Mkoa wa Dar es Salaam, Saimon Mwakifamba ametangaza  kuwa Octoba 5 mwaka huu kutakuwa na mkutano wa ndani wa wanachama wote , utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza, mapema leo katika ukumbi wa chama hicho, Mwakifamba anasema kuwa chama kimekaa na kuona kuwa kuna uhitaji wa kufanya mkutano utakao husisha wanachama wote wa chama hicho kuanzia ngazi ya shina. 

“Katika mkutano, Mgeni rasmi atakuwa Bashiru pamoja na Makamu wa Rais wa awamu ya tano ambaye ni mlezi wa chama hicho Samia Suluhu na viongozi mbalimbali wa chama, mkutano utafanyika katika uwanja wa taifa”amesema Mwakifamba. 

Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu Yusuph Nassor, amesemakuwa mkutani huo utahudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho na kuzungumzia yaliofanyika katika chama na yatakayotendeka.  

Aidha Mwenyekiti wa Vijana wa chama Dar es Salaam Musa Kilakala, ameongezea kwa kusema kuwa ” Tunataka kuona na kuzungumzia nini kinachoendelea katika chama chetu haswa wakati huu wa maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwezi ujao” .amesema
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles