Wenyeviti wanne upinzania wahamia CCM

0
1317
Ramadhani Machaku Zoa kati ya wenyeviti wanne wa mitaa wa Kibaya Kiteto, toka chama cha NCCR Mageuzi, akipokelewa kujiunga na CCM siku ya wazee duniani mjini Kibaya Kiteto.

Mohamed Hamad Kiteto

Wenyeviti wanne wa serikali za mtaa wa vyama vya upinzani mji mdogo wa Kibaya, wilayani Kiteto mkoani Manyara, wamejiuzulu na kujiunga na CCM kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano.

Wenyeviti hao ni Abubakari Kidevu (Chadema), Ramahaani Machamu Zoa (NCCR Mageuzi), Athumani Yusuph (Chadema) na Shabani Sendaro (CUF), ambao awali walichaguliwa na wananchi katika uchaguzi wa serikali za mitaa kipindi kilichopita.

Aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa wa Ngarenaro, Abubakari Kidevu amesema, amejiuzulu  kuunga mkono jitihada za Serikali ya CCM na kwamba haoni jipya kwenye chama alichoondoka.

“Sioni jipya Chadema sasa nimeona niungane na CCM ili tuweze kusonga mbele kimaendeleo kwani hakuna asiyefahamu kinachofanyika katika Serikali ya awamu ya tano za Magufuli, ni vyema tukawa pamoja,” amesema.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kiteto, Mohamed Kiyondo akiwapokea wanachama hao wapya toka vyama vya upinzani amesema haoni haja ya kuona watu wanaopinga Serikali na hasa ya awamu ya tano kutokana na kazi kubwa inayofanyika kuhudumia wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhandisi Tumaini Magesa akiwa katika sherehe hiyo amesema maamuzi ya wenyeviti hao ni sahihi hasa kwa kipindi hiki kutokana na mambo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano

“Serikali imeboresha huduma za jamii, imeweka heshima kwa mtawala na mtawaliwa, kuna miradi mikubwa ya Kitaifa, elimu, ujenzi wa barabara, huduma ya afya, haijapata tokea hivyo kwa mtu mwenye nia njema na Taifa lake, hana budi kuunga mkono Serikali ya Daktari John Pombe Magufuli,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here