SONAM KAPOOR, AHUJA KUFUNGA NDOA

0
719

CHEMBUR, INDIA


STAA wa filamu za Bollywood, Sonam Kapoor, ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii  kutangaza kuwa anatarajia kufunga ndoa mwaka huu.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 32, ametajwa kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa filamu ambao wanalipwa fedha nyingi kuliko msanii yeyote wa kike nchini humo.

Sonam aliweka wazi uhusiano wake na Anand Ahuja na sasa amedai jambo hilo la ndoa lipo kwenye mikakati ya kukamilika mapema iwezekanavyo.

Inasemekana kwamba wawili hao wanaweza kufunga ndoa wiki ya pili ya Mei mwaka huu, endapo kila kitu kitakuwa sawa kama walivyopanga.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here