24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

WIZKID, TIWA SAVAGE WAKANUSHA UHUSIANO

LAGOS, NIGERIA


MASTAA wa muziki, Wizkid na Tiwa Savage, wamekuwa wakihusishwa kuwa kwenye uhusiano, hivyo wawili hao wamedai hakuna chochote kinachoendelea zaidi ya urafiki.

Mashabiki wamekuwa na maswali mengi baada ya kuwaona wakiwa pamoja mara kwa mara, hasa sehemu za starehe, lakini Wizkid amedai muziki unawafanya wawe pamoja.

“Tiwa Savage ni rafiki yangu wa karibu sana, nimefanya naye kazi mbalimbali na tunaendelea kufanya kazi pamoja na ndiyo maana urafiki wetu unazidi kukua. Hatuwezi kufika huko ambako watu wanafikiri, lakini tunatarajia kufika mbali zaidi kutokana na muziki wetu,” alisema Wizkid.

Kwa upande wa Tiwa Savage, alisema: “Watu wanashtushwa na jinsi tulivyo karibu, hasa tukiwa kwenye jukwaa moja tunaweza hata kushikana, hiyo ni moja ya sanaa na si mapenzi kama watu wanavyodhani”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles