CAIRO, Misri
MBALI ya masomo mengine, wanafunzi wa sekondari nchini Misri watasoma kitabu kinachozungumzia maisha ya Mohamed Salah ili kiwape morali ya kufanikiwa kama alivyo staa huyo wa Liverpool.
Salah mwenye umri wa miaka 29, ana heshima kubwa katika taifa lake hilo kutokana na mafanikio yake kwenye soka, hivyo mamlaka zimeona zipige hatua moja mbele kwa kumweka kwenye mtaala wa elimu
Katika kitabu hicho, wanafunzi watajifunza namna Salah alivyochangia mafanikio ya timu ya taifa, klabu alizochezea, ikiwamo Liverpool, sambamba na alivyoshiriki kusaidia makundi mbalimbali kwenye jamii.
Kwa ngazi ya klabu pekee, Salah anayeitwa ‘Mfalme wa Misri’, ameifungia Liverpool mabao 140 tangu alipojiunga na miamba hiyo ya Anfield mwaka 2017.