28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Kurasini Heats kuikabili Brave Hearts ya Malawi

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

TIMU ya mpira wa kikapu ya Kurasini Heats kesho Oktoba 29,2021 inatarajia kuikabili Brave Hearts ya Malawi katika mchezo wa kwanza wa michuano ya kutafuta tiketi ya kucheza Ligi ya Kikapu Afrika kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Jumla ya timu ambazo ni mabingwa kutoka nchi wanachama wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Kikapu Ukanda wa Africa (FIBA Africa)

Kurasini Heats ambayo inawakilisha Tanzania, imepangwa kundi E na timu za City Oilers(Uganda), New Stars (Burundi) na Brave Hearts (Malawi).

Kundi D lina timu za Ulinzi Warriors (Kenya) Cobra Sport (South Sudan), Hawassa City (Ethiopia) Ascut (Madagascar).

Muonekano wa Uwanja wa Ndani wa Taifa utakaofanyika mashindano hayo, baada ya kufanyiwa ukarabati

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Oktoba 28,2021 kwenye Uwanja wa Ndani Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa, amesema mashindano hayo ni hatua ya awali ya kutafuta timu 16 zitazocheza Ligi ya Afrika.

“Ligi ya Afrika inaratibiwa na FIBA kwa kushirikiana na NBA kwa Bara la Africa ambapo timu bingwa toka kwenye nchi wanachama wa FIBA zitashindana katika hatua ya awali kufuzu kushiriki katika hatua ya timu 16 bora ambayo ndio ligi rasmi itachezwa.

“Ushiriki kwa Tanzania uwakilishi utafanywa na klabu ya Kurasini Heats ambayo ilifuzu kushiriki katika mashindano haya tangu mwaka jana 2020 ilipotwaa ubingwa wa Taifa wa Ligi ya Kikapu (National Basketball League-NBL),” amesema Magesa.

Amefafanua kuwa mashindano hayo yatafikia tamati Oktoba 31,2021 ambapo mchezo wa kesho wa ufunguzi utaanza saa 2:00 usiku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles