25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Somalia yamfukuza balozi wa UN

MOGADISHU, SOMALIA

SERIKALI ya Somalia imemwamuru Balozi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini hapa, Nicholas Haysom kuondoka kwa tuhuma za kuingilia masuala ya ndani ya taifa hili.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje imesema Haysom hakaribishwi tena Somalia na hawezi kuendelea kuendesha shughuli zake.

Hatua hiyo imetokea baada ya balozi huyo kuandika barua akiihoji Serikali maswali mengi kuhusu hatua zilizochukuliwa wakati wa makabiliano yaliyotokea katika mji wa Baidoa, Jimbo la Kusini Magharibi.

Makabiliano hayo yalihusiana na kukamatwa kwa naibu kiongozi wa zamani wa wanamgambo wa al-Shabaab, Sheikh Mukhtar Robow Abu Mansur mwezi uliopita.

Haysom alikosoa kukamatwa na kuuawa kwa waandamanaji waliokuwa wakipinga kukamatwa kwa Roobow kati ya Desemba 13 na 15, mwaka jana.

Balozi huyo alikuwa amemwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani, Mohamed Abukar Islow na kuzungumzia uzito wa taarifa ambazo zilikuwa zimewahusisha wanajeshi wanaoungwa mkono na UN na kukamatwa kwa kiongozi huyo.

Barua ya Haysom pia ilizungumzia kukamatwa kwa watu 300 wanaodaiwa kushiriki maandamano kupinga kukamatwa kwa Robow huku wengine 15 wakiuawa.

Baadhi ya waandamanaji walizuiliwa kwa zaidi ya saa 48 na kisha kuachiwa baadaye kati ya Desemba 18 na 22.

Mjumbe huyo wa UN alisema kwamba usaidizi wa UN hutolewa kwa misingi ya kulinda haki za binadamu.

Hayo yanajiri huku Umoja wa Ulaya (EU) ukisitisha misaada kwa polisi wa Serikali ya Jimbo la Kusini Magharibi la Somalia kutokana na mzozo unaohusiana na kukamatwa kwa Robow.

Mbali ya EU, mataifa ya Ujerumani na Uingereza pia yamesitisha msaada wao kwa polisi wa jimbo hilo.

Serikali ya Somalia ilikuwa imemzuia Robow kuwania urais wa jimbo hilo Desemba 19 ikisema bado anakabiliwa na vikwazo vya kimataifa.

Serikali hiyo ilimuunga mkono waziri wa zamani wa nishati Abdiasis Laftagaren ambaye alishinda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles