24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

SOKO LA AJIRA LINAHITAJI UJUZI ZAIDI YA VYETI

 

Na ABDALLAH NG’ANZI  (TUDARCo)

KUNA wakati unatafakari namna mambo yanavyokwenda, hasa katika zama hizi za kidigitali. Moja ya jambo kuu linaloumiza vichwa vya wahitimu wengi  ni ukosefu wa ajira.

Ajira imekuwa changamoto si kwa Tanzania pekee bali duniani kwa ujumla.

Ripoti ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) inaonesha kuwa mwaka huu idadi ya watu wasio na ajira itaongezeka kwa asilimia 5.8(awali ilikuwa asilimia 5.7) na kufanya jumla ya watu wasio na ajira kufikia milioni 500.8 duniani .

Hili si jambo zuri kulisikia likitamkwa kwani ndoto za wasomi wengi ni kujiajiri au kuajiriwa na kufaidi kile ambacho wamekitafuta kwa jasho kwa zaidi ya miaka 18. Binafsi nimegundua kuwa zipo sababu ambazo zinawakosesha ajira vijana wengi, mojawapo ni ujuzi binafsi wa mtu ukiachana na vyeti alivyo navyo. Kwa mfano, mhitimu akiulizwa mbali na elimu aliyonayo ni kipi cha ziada alicho nacho?

Katika dunia ya sasa elimu si stashahada, shahada ya uzamili au uzamivu. Elimu ni namna gani unaweza kukabiliana na mazingira magumu ya ushindani. Kwa sasa kama Taifa tumeanza na soko la pamoja la Afrika Mashariki (EAC) lakini pia sisi tukiwa sehemu ya Taifa tunachanganyika na watu wa mataifa mengine. Kuna fursa nyingi tu zinazoweza kubadilisha maisha yetu.

Mathalani, mara nyingi watu wanauliza kozi gani inalipa. Ukweli ni kwamba kila kilichopo duniani ukiweza kukitumia vizuri na kwa maarifa kinalipa. Lakini pia lazima uelewe kuwa milango haipo wazi kana kwamba utaweza kupata kila kitu kama unavyotarajia, inahitaji uvumilivu na kuvuja jasho.

Mambo yamebadilika, kuna wasomi wengi wenye sifa wanazurura, sasa mwenzangu uliyehitimu juzi tu kama unadhani umefika basi ukweli ni kwamba bado una safari ndefu.

Soko la ajira la sasa haliangalii shahada wala stashahada, bali wewe ukiwa mwajiriwa utaleta mabadiliko gani chanya kulisaidia shirika au taasisi? Una ujuzi gani zaidi ya shahada yako? Ikifika hapo kuna mambo yanajitokeza

Je, una kitu gani kinachokutofautisha na washindani wengine? Wasomi msibweteke, endeleeni kutafuta ujuzi ili kujiongezea thamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles